Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu amesema kuwa bado hajapata taarifa kuhusu agizo la Rais John Magufuli kumpandisha cheo askari wa usalama barabarani aliyepambana na mke wa Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga.

Kwa mujibu wa ‘Nipashe’, IGP Mangu amesema kuwa hata kama atapata taarifa rasmi kuhusu agizo la hilo la Rais Magufuli, askari huyo atalazimika kwanza kwenda kwenye mafunzo kukidhi taratibu za Jeshi hilo.

“Bado hajapandishwa cheo kwa sababu sijapewa taarifa hizo na nitakapopewa taarifa atalazimika kwenda kwenye mafunzo kwanza, sisi jeshi la polisi tuna taratibu zetu,” IGP Mangu ananukuliwa.

Hivi karibuni, Rais Magufuli aliagiza koplo Deogratius Mbango apandishwe cheo kutokana na kusimamia sheria alipolikamata gari lililokuwa limemba mke wa Waziri Mahiga.

Magufuli akubali Kuyabeba mazito ya Kikwete
Waziri Mahiga atoa ya moyoni kuhusu sakata la mkewe na trafiki