Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Bi. Juliet Kairuki ambaye amezua maswali baada kuonekana hajawahi kuchukua mshahara wake tangu Aprili mwaka 2013.

Taarifa ya kuondolewa kwa Bi. Kairuki iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda imeeleza kuwa Rais amechukua hatua hiyo tangu Aprili 24 mwaka huu.

Hata hivyo, Rais amempa nafasi ya kupangiwa kazi nyingine endapo atakuwa tayari kuendelea kufanya kazi na Serikali ya awamu ya Tano.

TIC

Gonzalo Gerardo Higuaín Awekwa Sokoni Rasmi
Muswada kuhusu zuio la Ndoa kwa hawa... kutua bungeni