Rais John Magufuli ambaye anafahamika pia kama ‘mtumbua majipu’, huenda akalazimika kuwatumbua majipu baadhi ya mawaziri wake baada ya kubainika kuwa wamekiuka sheria ya maadili ya utumishi wa umma.

Mawaziri hao wenye ‘majipu’ wamedhihirika jana baada ya kuwekwa wazi na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Salome Kaganda Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa semina ya siku moja kwa mawaziri na Naibu mawaziri kuhusu sheria ya maadili, mgongano wa maslahi na mwongozo maadili ya vionzogozi wa umma na utekelezaji wa ahadi ya uadilifu.

Jaji Kaganda alieleza kuwa baadhi ya mawaziri na naibu mawaziri hawakujaza fomu za tamko la mali, maslahi na madeni pamoja na uadilifu, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria ya maadili ya utumishi wa umma.

Alisema kuwa Sekretarieti yake itayakabidhi majina ya Mawaziri na naibu Mawaziri hao kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa ajili ya kuchukuliwa hatua stahiki za kiutawala na kisheria.

“Waziri Mkuu ameshakisaini kiapo hiki na amekitundika ukutani ofisini kwake anakisoma mara kwa mara. Naanyi mnatakiwa kiga, kutosaini ni wazi kuwa mnapinga sheria hii,” alisema Jaji Kaganda.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwawajibisha watumishi wasiofuata maadili kwani wapo watu wengi nchini ambao wanania ya kutumikia taifa kwa moyo wa dhati na uaminifu.

Januari mwaka huu, Rais John Magufuli aliwaapisha Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu wakuu, ambapo aliwaagiza kusaini kiapo cha maadili huku akimpa nafasi yeyote anaeona ugumu kujaza kiepengele chochote kwenye fomu hiyo kuengua mapema.

Wasira: Nilianza kupigwa picha tangu natoka chooni, nahisi huyu katumwa
Bashe aitahadharisha Elimu Bure ya Magufuli