Mahakama Kuu ya Zanzibar iliyopo Chake Chake, Kisiwani Pemba imemhukumu kunyongwa hadi kufa Askari Polisi, Erick Nangomo baada ya kupatikana na hatia ya kuwaua wenzake wawili.

Aidha katika kesi hiyo iliyoongozwa na Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Abraham Mwampashi, imethibitika kuwa Nangomo aliwauwa Polisi wenzake kwa kuwapiga risasi kwa makusudi.

“Kutokana na mshtakiwa kubainika na kosa la kuua kwa makusudi, Mahakama haina haja ya kusikiliza kumbukumbu za makosa na haitosikiliza utetezi kutoka kwa wakili wake,”amesema Mwampashi.

Polisi huyo alishtakiwa kwa makosa mawili tofauti ambayo ni kutumia silaha kuwaua wenzake, kwa kukusudia juni 20, 2003 saa 11:58 jioni katika kituo cha Polisi Chake Chake.

Hata hivyo, Jaji ameiambia Mahakama kuwa kosa hilo alilolifanya ni kinyume na kifungu cha 180 na 181 cha sheria namba 13 sheria ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Gali la Mbunge laua, yeye anusurika
Makonda aomba viongozi wa dini kuendeleza kuamrisha mema, aombewa dua