Mahakama Kuu Kanda ya Dar  es Salaam, jana ilimuagiza Kamanda wa Polisi Kanda ya Ilala kumkamata Meneja wa msanii Diamond,  Hamis Taletale maarufu kama Babu Tale.

Mahakama Kuu imetoa amri hiyo jana kutokana na Babu Tale kutotii amri ya mahakama hiyo iliyomtaka kumlipa Sheikh Hamis Mbonde shilingi milioni 250 kwa kusambaza DVD za mawaidha yake bila idhini yake, kinyume na sheria ya haki miliki.

Katika shauri hilo lililotajwa jana mbele ya Kaimu Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Juma Hassan, Babu Tale na mdogo wake Iddi Tale walitajwa kukaidi amri ya mahakama ilitolewa Februari 18 mwaka huu ikiagiza wamlipe sheikh Mbonde kiasi hicho cha fedha.

Imeelezwa kuwa Julai 8 mwaka huu, Mahakama hiyo ilitoa amri ya kukamatwa kwa wadai hao ambao walitakiwa kufikishwa mahakamani hapo jana lakini agizo hilo halikutekelezwa, hivyo jana iliamua kutoa agizo hilo kwa mara  nyingine kwa Kamanda wa Polisi Kanda ya Ilala.

Wawili hao wanatakiwa kufikishwa tena Mahakamani kujitetea kwanini Mahakama hiyo isiwape adhabu ya kukiuka amri ya Mahakama.

Juan Mata Kubaki Old Trafford
Wizara Ya Maliasili Na Utalii Yatakiwa Kujipanga