Kiungo kutoka nchini Hispania Juan Mata amepata uhakika wa kuendelea kusalia Man Utd, baada ya kuthibitishiwa na meneja wa klabu hiyo Jose Mourinho.

Mata alikua katika hali ya sintofahamu baada ya meneja huyo kutoka nchini Ureno kutangazwa kuwa mrithi wa Louis Van Gaal, kutokana na mara zote amekua hakubaliki katika mfumo wa Mourinho.

Baadhi ya vyombo vya habari vilizua mjadala kwa wawili hao kupika chungu kimoja, baada ya kutibuana walipokua Stamford Bridge na kufikia hatua Mourinho kumuuza Mata kwenye klabu ya Man Utd msimu wa 2013-14, kwa ada ya Pauni milioni 34.

Mourinho hakuamini uwezo wa Mata, katika falsafa za kucheza nafasi ya kiungo mkabaji kama ilivyokua kwa viungo kutoka nchini Brazil Oscar na Willian ambao aliwabadilisha na kuwafanya kuwa na uwezo wa kuzuia na kushambulia.

Kwa sasa Mourinho amekua akifanya kazi na Mata kwa kujaribu kumtumia kama kiungo ambaye atapaswa kucheza katika nafasi ya kukaba na kuzuia kwa wakati huo huo, jambo ambalo linaonyesha huenda likazaa matunda.

Tayari baadhi ya vyombo vya habari vilianza kutoa nafasi kwa Juan Mata kuihama Man Utd na kwenda kujiunga na klabu ya Everton, kufuatia meneja wa The Toffees, Ronald Koeman kutamka hadharani kuhitaji huduma ya kiungo huyo.

Maji yawafika kooni viongozi CCM waliokwepa kumpokea Magufuli akiomba udhamini
Mahakama yaagiza Babu Tale akamatwe, atakiwa kumlipa sheikh milioni 250