Ikiwa zimebaki siku tatu tu Rais John Magufuli akabidhiwe rasmi Uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), hofu ya baadhi ya viongozi wa chama hicho wanaodaiwa kumkwepa wakati lipokuwa akipita kuomba udhamini katika mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM inadaiwa kupanda.

Taarifa kutoka Mjini Dodoma zimeeleza kuwa wakati kazi ya kuendelea kuwabaini viongozi na wanachama waliokisaliti chama hicho katika uchaguzi Mkuu uliopita ikiendelea ili waweze kuchukuliwa hatua na Mwenyekiti mpya, imebainika kuwa baadhi ya wenyeviti wa wilaya na mikoa walikuwa wakimkimbia Dk. Magufuli alipofika kuomba udhamini kwasababu alikuwa hatoi fedha (takrima) huenda wakashughulikiwa.

Hayo yamebainishwa na ripota wa Clouds Fm mapema leo asubuhi kwenye kipindi cha Power Breakfast, ambaye amepiga kambi mjini humo kwa ajili ya kuripoti matukio ya mkutano  Mkuu Maalum wa chama hicho.

“Inaelezwa kuwa baadhi yao walikuwa wakimsikia anakuja wanamkwepa, hawaendi ofisini.. wanasiwa kuwa walikuwa wanamkwepa kwa sababu yeye alikuwa hatoi fedha,” alisema ripota huyo.

Rais Magufuli ambaye alitangaza kuchukua fomu ‘kimyakimya’ na kuzunguka kutafuta wadhamini ‘kimyakimya’ pamoja na kuirejesha ‘kimyakimya’, aliibuka kuwa mshindi bila kutarajiwa na wengi.

Saa chache baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu mwaka jana, Rais Magufuli aliahidi kuwashughulikia wasaliti wa chama hicho.

Rafael Benitez Aitega Liverpool
Juan Mata Kubaki Old Trafford