Kesi ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe dhidi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kupinga kuondolewa katika jengo la shirika hilo imechukua sura mpya baada ya Msajli wa Mahakama kukana kuitambua kampuni ya Fosters Auctioneers and General Traders ilitumika kumuondoa.

Kampuni hiyo ya udalali ambayo NHC iliipa tenda ya kumuondoa Mbowe na kupiga mnada vitu vyake ili kufidia deni la shilingi bilioni 7 baada ya kumtaja kama mdeni sugu, uamuzi ambao umezuiwa kwa muda na mahakama ili kupisha kusikilizwa kwa maombi ya mlalamikaji na kesi ya msingi.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Wakili anayemtetea Mbowe, Peter Kibatala alisema kuwa waliwasilisha barua kwa Msajili wa Mahakama kutaka kujua uhalali wa kampuni hiyo kwani makampuni ya  yanayofanya shughuli hizo husajiliwa mahakamani, lakini walijibiwa kuwa haliko kwenye orodha ya makampuni yaliyosajiliwa mahakakani hapo.

Kibatala aliwasilisha barua hiyo ya Msajili wa Mahakama katika Mahakama Kuu inayosikiliza kesi hiyo na kueleza kuwa kwa mujibu wa majibu hayo, yote yaliyofanywa dhidi ya mteja wake sio halali kisheria.

Mbowe anaiomba Mahakama hiyo iamuru NHC na Kampuni ya Fosters Auctioneers and General Traders kurejesha vitu vyake kwenye jengo walilomtimua kwani walifanya hayo kinyume cha sheria.

Akizungumzia madai ya kutotambulika kwenye orodha ya makampuni iliyosajiliwa na Msajili wa Mahakama, Wakili wa kampuni hiyo, Aliko Mwamanenge alisema kuwa Mteja wake ni dalali aliye chini ya Baraza la Usuluhishi na kwamba anayesajiliwa kama dalali ni mtu binafsi na sio Kampuni.

Mahakama Kuu imeahirisha kesi hiyo na imepanga kutoa uamuzi wake Oktoba 18 mwaka huu.

Mama Diamond (Bi Sandra) amtakia Wema Sepetu Happy Birthday
Mwalimu amtia mimba mtoto wa darasa la 4, atuhumiwa kifungo cha miaka 32