Mahakama ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, hii leo Aprili 5, 2023 imemuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, baada ya kukiri makosa yake yaliyokuwa yakimkabili kwa njia ya makubaliano maalumu.

Makubaliano hayo yanatokana na kesi ya jinai kati ya Mwendesha Mashtaka na Mshitakiwa ambapo Mshitakwa anaweza kukubali kukiri kosa moja au zaidi kwa aliyoshitakiwa ili apate nafuu katika kesi inayomkabili.

Lengai Ole Sabaya akishuka kwenye gari katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Kilimanjaro hii leo,  Aprili 5, 2023. Picha ya Janeth Joseph

Machi 29, mwaka akiwa Mahakamani hapo, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Sabitina Mcharo aliieleza Mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo namba mbili ya mwaka 2022 umekamilika na kuiomba Mahakama kuwapa tarehe ya karibu kwa ajili ya taratibu nyingine za kisheria.

Washtakiwa wengine wanne, Sylivester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Assey waliachiliwa huru Septemba 6, 2022 baada ya kukiri makosa na mahakama iliwatia hatiani na kuwaamuru kulipa kila mmoja faini ya Shilingi 50,000 na fidia ya Shilingi 1 milioni kwa mwathirika wa tukio Alex Swai.

Uaminifu sekta ya Madini utakuza uchumi wa Taifa: Waziri Biteko
Miundombinu barabara za utalii Kilimanjaro yaimarishwa