Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amemuagiza mmiliki wa mgodi wa dhahabu wa Namungo kufika Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma Septemba 10, 2021 ili kuelezea mipango yake ya kuendeleza mgodi huo pamoja na wachimbaji wadogo.

Aidha Waziri Mkuu Majaliwa ameutaka uongozi wa mgodi huo uhakikisha wanaweka mazingira mazuri yatakayowawezesha wachimbaji wadogo kunufaika.

Hayo yamejiri leo Agosti 20, 2021 baada ya kutembelea mgodi huo uliopo wilayani Ruangwa, Lindi akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za maendeleo.

Naye, Naibu Waziri wa Nishati Profesa Shukuru Manya, amesema Serikali imeweka mikakati madhubuti ili kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali ya madini iliyoko nchini.

Kwa upande wake, Meneja wa Kampuni Lindi Jumbo inayochimba madini ya graphite Paul Shauri amesema mgodi huo utaanza kuzalisha ifikapo Agosti, 2022.

Balozi Mulamula atoa angalizo kwa wanadiplomasia
Boss wa zamani wa ATCL na wenzake wahukumiwa