Viongozi na wananchi wa Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar wametakiwa kushiriakiana kwa pamoja ili kuweza kuimarisha na kuulinda Muungano ulioachwa na waasisi wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mapema hii leo  Zanzibar mara baada ya kushiriki hitma na kuzuru kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Sheikh Abeid Karume lililoko  Qfisi Kuu za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui Mjini Unguja

Amesema kuwa Watanzania wote Bara na Visiwani ni wamoja kiasili, hivyo wanapaswa kushirikiana ili kuweza kujiletea maendeleo na kuhakikisha kwa pamoja kuulinda na kuudumisha Muungano ulioachwa na waasisi wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Karume.

“Tuhakikishe Muungano huu tulioachiwa na waasisi wa Taifa letu unadumu ili tuendelee kuwa wamoja na kuzungumza lugha moja ya kuboresha maendeleo na kulinda amani na utulivu wa nchi yetu,” amesema Majaliwa.

Aidha, Majaliwa amesema katika kutambua umuhimu wa viongozi hao Serikali imetenga siku maalumu kwa ajili ya maadhimisho ya vifo vya viongozi hao na kutoa fursa kwa wananchi kila mtu kwa imani yake kuwaombea dua na kutafakari namna walivyojitoa kwa taifa letu.

Vile vile, Maadhimisho hayo ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Karume hufanyika kila Aprili 7 ya kila mwaka na Hayati Mwalimu Nyerere ni Oktoba 14 ya kila mwaka.

Hata hivyo, Maadhimisho hayo ya kifo cha Sheikh Karume yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd.

Wengine ni Rais Mstaafu wa awamu ya Pili,  Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Amani Abeid Karume, Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilal, wazee wa CCM pamoja na wananchi

Wizara ya Habari yatoa tamko kuhusu kupotea kwa msanii 'Roma'
Wadau wa michezo wapewa siri ya mafanikio, watakiwa kuijtokeza