Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo imekanusha taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa msanii aliyepotea, Ibrahim Mussa maarufu kwa jina la ‘Roma Mkatoliki’ kuwa anashikiliwa na Polisi.

Aidha, katika taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Zawadi Msalla imesema kuwa Wizara kwa dhamana yake katika tasnia ya Sanaa imepokea kwa mshtuko taarifa za kutoweka kwa Mwanamuziki huyo tangu tarehe 5 Aprili 2017.

Katika taarifa hiyo, Msalla amesema kuwa Wizara imefuatilia kwa karibu suala hilo kwa kuwa lina mwelekeo wa kosa la jinai, hivyo amesema taarifa kutoka kwa vyombo vya dola zinathibitisha kuwa Roma Mkatoliki hashikiliwi katika kituo chochote cha polisi.

Hata hivyo, Kutokana na uzito wa jambo hilo amesema kuwa, Wizara inawaomba wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuweza kutoa taarifa zozote zitakazo saidia kujua mahali msanii huyo.

Ray C afunguka mpango wa ‘kuvamia Media’ na alivyojipanga
Majaliwa atoa ujumbe mzito kwa Watanzania