Kocha Kali Ongala ataendelea kubaki mkuu  wa benchi la ufundi la Majimaji.

Tayari Kali alikuwa amemalizana na Azam FC na alitarajia kujiunga na timu hiyo leo kwa ajili ya safari ya Zanzibar.

Azam FC iliamua kumchukua Kali kwa kuwa imemfukuza kocha wake Zeben Hernandez na jopo zima kutoka Hispania.

Lakini Majimaji chini ya uongozi wa kampuni GSM, imefanikiwa kumbakiza Kali.

Habari za uhakika kutoka Majimaji zimeeleza, uongozi wa klabu hiyo umefanikiwa kumshawishi Kali kubaki.

“Kweli Kali anabaki na ataendelea kuwa kocha wa Majimaji,” kilieleza chanzo.

“Juzi aliwaaga wachezaji kwa kuwa alikuwa ameishazungumza na Azam FC. Lakini baadaye uongozi umemuita na umefanikiwa kumshawishi abaki.”

Kuhusiana na Kali, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba alisema bado wako kwenye mazungumzo na Majimaji ili kumtwaa.

Tony Pulis: Arsenal Wana Kikosi Bora Kuliko Chelsea
Video: Majambazi wengi wanaotumia silaha wamekamatwa - Sirro