Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema hataki watumishi mizigo katika mkoa wake na kuongeza kuwa hatowahamisha watumishi waliofanya kazi kwa mda mrefu mpaka watakapo timiza majukumu yao waliyopangiwa ya kuwahudumia wananchi.

Ameyasema hayo katika muendelezo wa ziara yake katika Wilaya ya Ilala baada ya kuhitimisha ziara yake jana Wilaya ya Temeke.

Kabla ya kunza ziara yake, Makonda amefanya mazungumzo na watumishi wa Idara mbalimbali wa Halmashauri ya Ilala na kusisitizia suala la uwajibikaji.

“Watumishi mizigo katika Mkoa wangu siwataki,na kuna wale waliofanya kazi kwa muda mrefu sitawahamisha mpaka watakapotimiza majukumu yao kwa wananchi.alisema Makonda.

Hata hivyo, Makonda amesema kuwa kufanya kazi kwa muda mrefu inabidi kuendane na uwajibikaji bora wenye manufaa na tija kwa Taifa na wananchi, vilevile ametoa tahadhali kwa watumishi waliopata nafasi za ajira kupitia watu flani wajiandae kwani amejipanga kuwawajibisha kama wasipo jiwajibisha.                                                                                                                                                                                                                                                                                 Kwa upande wake Katibu Tawala wa Halmashauri ya Manispaa ya  Ilala, Edward Mpogolo  amemuomba, Makonda kutoa kipaumbele kwa wilaya ya Ilala, kwa kuongeza vituo vya Afya, na vituo vya Polisi kama alivyopanga  kuongeza vituo 20 kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Video: Waliozuia Mkutano wa Maalim Seif ni viongozi wa Mtwara, Alienda na ajenda mbovu - Prof. Lipumba
Maadhimisho ya kupinga ukatili wa kijinsia kuanza Novemba 25