Klabu za Manchester United na Chelsea zote za nchini England zimeimngia katika ushindani wa kumuwania mshambuliaji kutoka Brazil na klabu ya Santos Gabriel Barbosa pamoja na kiungo Thiago Maia.

Wawili hao wameingia katika rada za klabu hizo ambazo mwishoni mwa juma hili zitaanza harakati za kuwania ubingwa wa nchini England, huku wakiwa katika majukumu ya kuitumikia timu yao ya taifa katika michuano ya Olimpiki inayoendelea nchini Brazil.

Klabu za Leicester City pamnoja na Inter Milan ziliwahi kuwasilisha ofa ya Pauni milioni 23 kwa nia ya kutaka kumsajili Barbosa, lakini uongozi wa Santos ulionyesha kutokua na haraka ya kumuachia kinda huyo mwenye umri wa miaka 19, kwa kusubiri ofa kubwa ambayo wanaitarajia.

Gabriel Barbosa has scored twice for Brazil at the OlympicsGabriel Barbosa

Rais wa klabu ya Santos, amesema alikutana na viongozi wa klabu za Man Utd pamoja na Chelsea nchini Hispania na wameonyesha kuwa tayari kuwasajili wachezaji hao wawili ambao huenda wakabadili mazingira ya kucheza soka lao kuanzia msimu huu wa ligi.

Barbosa, ambaye tayari ameshafunga mara mbili katika michuano ya Olimpiki, amekua na nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha Santos na anaonyesha kiwango kizuri cha kuisaidia klabu hiyo katika harakati za kuuwania ubingwa wa nchini Brazil, huku Maia mwenye umri wa miaka 19 akifuata nyendo hizo, na mpaka sasa ameshaanzishwa katika kikosi cha kwanza mara 44 tangu alipopandishwa akitokea kwenye kikosi cha vijana tangu mwaka 2014.

Moussa Sissoko Aendelea Kuiota Real Madrid
England Kujipima Kwa Mabingwa Wa Dunia Wa 2010