Kiungo wa Man Utd, Michael Carrick ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England ambacho hii leo kitakua na shughuli ya kupambana na timu ya taifa ya Uswis kwenye uwanja wa Wembley jijini London.

Carrick amerejeshwa mjini Manchester, baada ya kubainika anasumbuliwa na matatizo la kiazi cha mguu kufuatia vipimo alivyofanyiwa mapema hapo jana.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson amethibitisha taarifa za kuumia kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34, kwa kusema Carrick alipatwa na maumivu hayo alipokua kwenye mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa hii leo.

Hatua hiyo inakua bahati mbaya kwa Michael Carrick, kutokana na ndoto zake za kutaka kuendelea kuitumikia timu yake ya taifa kufifia siku hadi siku, kwani kwa mara ya mwisho aliwahi kufanya hivyo wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Italia uliomalizika kwa sare.

Kuumia kwa Carrick kutamfanya akae nje na kushuhudia wachezaji wenzake wa Man Utd wakipambana mwishoni mwa juma hili katika mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England dhidi ya Liverpool.

Venus Williams Atamba Kumaliza Uteja Kwa Serena
CCM Wapata Silaha Nyingine Dhidi Ya Lowassa