Chama cha mapinduzi CCM wameendelea kutafuta namna ya kuwashawishi zaidi watanzania kutomchagua mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa ili kumpa nafasi zaidi mgombea wa chama hicho, Dk John Magufuli.

Hivi karibuni, timu ya CCM ya mitandao ya kijamii iliibua kipande cha video kinachomuonesha Lowassa akiwa ndani ya kanisa la Kirutheri akizungumza na waumini wa kanisa hilo ambapo alidai kuwa ‘awamu hii rais atatoka katika kanisa hilo’.

“Naomba mniombee, Mniombee kwelikweli, nyie walutheri mnasababu ya kuomba zaidi. Kwa sababu nchi hii tangu iumbwe haijawahi kupata mlutheri kuwa rais. Mwalimu Nyerere alikuwa Mkatoliki, Mkapa alikuwa Mkatoliki, sasa nadhani Mungu anatuongoza vyema. Kwa hiyo naomba mniombee sana,” Lowassa anawaambia waumini wa kanisa hilo.

Mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM, January Makamba amepost kipande hicho cha video kwenye Twitter na kueleza jinsi alivyoshangazwa na maelezo ya Lowassa.

“Lowassa tells a Lutheran congregation that country needs a Lutheran President. Politics aside, how dangerous is this?” Alitweet January Makamba.

Man Utd Kuikabili Liverpool Bila Michael Carrick
Kalusha Bwalya Awapigia Chapuo Makocha Wazawa