Magwiji wa soka mjini Manchester, Man Utd wameacha mshangao kwa wadau wengi wa michezo duniani kote, baada ya kutoa tangazo la ziara yao ya mashariki ya mbali (China) ambayo itaambatana na michezo ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi, bila ya kuwepo kwa Louis van Gaal.

Man Utd wametoa tangazo hilo hii leo, ambapo maswali mengi bado yameendelea kuchakata kwa walio wengi, kwa kujiuliza kwa nini Van Gaal hayupo katika mpango huo.

Sio kawaida kwa Man utd kumuweka pembeni meneja huyo kutoka nchini Uholanzi, tangu alipotangazwa kuwa kiongozi wa benchi la ufundi mwaka 2014 huko Old Trafford, na alikua akionekana katika matangazo ya maandalizi ya misimu iliyofuatia.

Hata hivyo hisia zimeanza kuibuka miongozi wa wadau wa michezo kwa kuamini huenda kazi kwa mzee huyo mwenye umri wa miaka 64, ikawa inaishia mwishoni msimu huu, kutokana na tetesi nyingine kuzungumzia ukomo wake kufuatia mambo kumuendea hovyo tangu alipowasili.

Katika ziara hiyo, Man Utd, watapambana na mahasimu wao wa mjini Manchester, Man City pamoja na Borussia Dortmund katika michuano ya kombe la mabingwa wa kimataifa (International Champions Cup) itakayofanyika mjini Beijing na Shenzhen mwezi July.

Man Utd watacheza mchezo wao wa kwanza katika uwanja wa Bird’s Nest Julai 25.

Waziri Maghembe amtumbua Mkurugenzi Wanyamapori kwa kuvusha Tumbili
Stars Kurejea Dar Usiku Wa Manane