Siku kadhaa baada ya kumthibitisha Jose Mourinho kama meneja wao mpya, uongozi wa Manchester United umetangaza kuanza mikakati ya kufanya maboresho ya kikosi chao kwa kuhakikisha wanawasajili wachezaji waliokusudiwa.

Pendekezo la kwanza katika usajili wa klabu hiyo nguli nchini England, ni kiungo wa klabu bingwa nchini Italia, Juventus Paul Pogba ambaye amekua akiwindwa na klabu nyingine barani Ulaya hususan FC Barcelona ya Hispania.

Jose Mourinho, ameonyesha dhamira ya kutaka kumsajili kiungo huyo, kufuatia jina lake kuonekana katika orodha aliyoiwasilisha kwa mtendaji mkuu wa Man Utd, Ed Woodward.

Meneja huyo kutoka nchini Ureno, amesisitiza kusajiliwa kwa kiungo huyo ambaye thamani yake ni Pauni milioni 76, kwa kuamini endapo akikamilishiwa mpango huo mambo yatamuendea vyema msimu ujao wa ligi.

Hata hivyo Pogba mwenye umri wa miaka 23, bado amesaliwa na muda wa miaka mitatu katika mkataba wake na klabu ya Juventus na hajawahi kuzungumza suala lolote kuhusu kutaka kuondoka Juventus Stadium.

Kama Mourinho atakamilishiwa mpango wa kusajiliwa kwa kiungo huyo, atakuwa amefanikisha mikakati ya kumrejesha Pogba Old Trafford, ambapo alikuzwa na kuendelezwa kisoka, kabla ya kuamua kuondoka mwaka 2012, baada ya kukataa kusaini mkataba mpya.

Wachezaji wengine wanaotajwa kuwa kwenye orodha ya Jose Mourinho ni kiungo wa Willian (Chelsea) kiungo wa Saul Niguez (Atletico Madrid)  pamoja na mshambuliaji aliye huru kwa sasa  Zlatan Ibrahimovic.

Spurs Kumsajili Mfaransa ili Kumpa Pressue Harry Kane
Roberto Di Matteo Kukabidhiwa Zigo La The Lions