Klabu ya Tottenham imeripotiwa kuwa katika mazungumzo na uongozi wa Olympic Lyon kwa ajili ya kufanya biashara ya mshambuliaji Alexandre Lacazette mwenye thamani ya Pauni milioni 30.

Mtendaji mkuu wa Spurs, Daniel Levy amekua shabiki mkubwa wa mshambuliaji huyo na kwa bahati nzuri amepata ushirikiano kutoka kwa meneja wa klabu hiyo ya kaskazini mwa jijini London, Mauricio Pochettino ambaye pia anahitaji kuona anafanya kazi na Lacazette.

Levy yupo mjini Lyon nchini Ufaransa kwa ajili ya kuweka mambo sawa ya usajili wa Lacazette ambaye msimu uliopita alifanikiwa kufunga mabao 23 ambayo yalisaidia kuifikisha klabu yake kwenye nafasi ya pili na kumaliza ligi kwa tofauti ya point 31 dhidi ya mabingwa PSG.

Tottenham wameanza mikakati ya kumuwania mshambuliaji huyo wa kifaransa, wakiwa na lengo la kumtafutia Harry Kane mbadala wake ambaye atampa motisha ya kupambana wakati wote.

Drinkwater Amtumia Ujumbe Mzito Kocha Wa England
Man Utd Ya Jose Mourinho Kuanza Na Paul Pogba