Kiungo wa klabu bingwa nchini England, Leicester City Danny Drinkwater ameonekana kusikitishwa sana baada ya jina lake kuenguliwa katika kikosi cha timu ya taifa ya England kitakachoshiriki michuano ya Euro 2016 nchini Ufaransa.

Kiungo huyo ambaye ndiye amepiga ‘tackles’ nyingi kwenye ligi ya EPL msimu huu ulioisha (103), mara ya kwanza aliitwa kikosi cha awali cha wachezaji 26. Hata hivyo baada ya Roy Hodgson kutangazaa kikosi cha mwisho chenye wachezaji 23, jina lake halikuwemo.

Drinkwater ambaye ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kabisa kuitwa kwenye kikosi hicho, alicheza mchezo wake wa kwanza mwezi March dhidi ya Uholanzi.

Hata hivyo ameshindwa kuzuia hisia zake baada ya kutemwa na katika kikosi hicho – kitu ambacho kimsingi kinatia mashaka ukizingatia ubora aliounesha katika klabu na kuchangia kuipa ndoo ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.

Ameandika hivi;

Disappointed not to make the final 23! Would of been a fantastic experience to go to the euros as a player… But I’ll be supporting the country like I always have! The seasons been a huge positive for me.. Going into next season as a premier league champion! Good luck to the lads… Bring it home ?? #england”

Anamaanisha hivi: “Nimefedheheshwa sana kutojumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 23!ingekuwa ni jambo kubwa sana kwangu kwenda Euro nikiwa kama mchezaji….lakini nitakuwa nikiisapoti nchini yangu ambayo ndiyo inanihusu!msimu wa ligi uliosha ulikuwa ni mzuri sana kwangu….nikijiandaa kwenda msimu mpya kama bingwa wa EPL!Muwe na baraka nyingi ndugu zangu… hakikisheni kombe linakuja nyumbani#england”.

Mourinho: Sitathubutu Kupoteza Muda Kwa Kumfikiria Pep Guardiola
Spurs Kumsajili Mfaransa ili Kumpa Pressue Harry Kane