Klabu ya Manchester United ina mpango wa kuwasilisha ofa ya Pauni Milioni 50 kwenda Real Madrid ili kuipata saini ya beki wao kisiki kutoka nchini Ufaransa, Raphael Varane.

Varane mwenye umri wa miaka 28, amekua kwenye rada za Man Utd kwa muda mrefu, na sasa klabu hiyo imejizatiti kumchukua jumla jumla.

Mbali na Varane, Man Utd inajipanga kuwasilisha ofa ya Pauni Milioni 25 kwenda Rennes ili kuipata saini ya kiungo Mfaransa Eduardo Camavinga mwenye umri wa miaka 18, katika kipindi hiki cha dirisha la usajili.

Nguvu ya usajili kwa wawili hao imewekezwa huko Old Trafford, baada ya kukamilishwa kwa dili la usajili wa Sancho juma lililopita.

Hata hivyo, kwa upande wa Camavinga ofa hiyo haionekani kuwa inaweza kukubaliwa kutokana na lundo la timu zinazohitaji huduma yake tena kwa ofa nono.

Man United ipo kwenye mchakato wa kusuka upya kikosi chao baada ya kutofanya vizuri msimu uliopita.

Manara atimiza ahadi, akutana na Mzee Mpili
Habari Mpasuko: Balotelli atua Adana Demispro