Hatimaye Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC Haji Sunday Ramadhan Manara, ametimiza ahadi ya kumkabidhi Shilingi Milioni Moja (1, 000, 000) Mwanachama Mfurukutwa na Mkereketwa wa Young Africans Mzee Mpili.

Haji aliahidi kumpa Shilingi Milioni Moja Mzee huyo, endapo Young Africans ingeshinda dhidi ya Simba SC, jambo ambalo lilitokea siku ya Jumamosi (Julai 03), Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.

Manara ametimiza ahadi yake kwa kumkabidhi Mzee Mpili mzigo wake leo Jumatano usiku (Julai 07) nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es salaam.

Kabla ya kuthibitishiwa uhakika wa kuipata Milioni Moja, Mzee Mpili alimtaka Haji Manara kutimiza ahadi yake mapema juma hili aliposhiriki kwenye kipindi cha ‘KIDEO SOKA’ cha Dar24 Media ambacho kilirushwa hewani Jumatatu jioni.

Chombo cha habari cha Dar24 Media ndicho kilimuibua Haji Manara baada ya kuzungumza na Mzee Mpili mapema juma lililopita na kumuuliza maisha halisi ya Msemaji huyo wa Simba SC (Kabla na baada ya kuzaliwa kwake).

Manara alikubaliana na yote yaliosemwa na Mzee Mpili hasa suala la Mzee Manara kupata changamoto alipokwenda kumposa mama yake Haji.

Kimahesabu Simba SC Bingwa 2020/21
Man Utd yajifunga kibwebwe usajili wa Varane, Camavinga