Uwezekano wa wachezaji Khalid Aucho, Djuma Shaban na Fiston Mauele kuukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, umeongezeka maradufu kufuatia ukimya uliotawala kutoka Shirikisho la soka Barani Afrika ‘CAF’.

Wachezaki hao watatu mpaka sasa hawajapata vibali vya uhamisho wa kimataifa ambavyo vinapaswa kutumwa nchini na vilabu vilivyokua vinawamiliki kabla ya kutua Young Africans.

Msemaji wa Young Africans Haji Sunday Manara amesema mpaka sasa hakuna taarifa yoyete kutoka CAF kuhusu wachezaji hao.

Amesema Young Africans itaendelea kusubiri hadi vibali vyao vitakapopatikana, na ndipo benchi la ufundi litakuwa na uhuru wa kuwatumia.

“Mpaka sasa CAF waki kimya juu ya suala hili, hawajatuambia lolote kuhusu ITC za Djuma Shaban, Aucho na Mayele, hivyo tunaheshimu taratibu za kutowatumia kwenye mchezo dhidi ya Rivers United Jumapili (Septemba 12).”

Young Africans itakuwa mwenyeji wa Rivers United katika mchezo huo wa hatua ya awali wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam Jumapili (Septemba 12).

Tozo mpya yamuamsha Spika
Suluhu yapatikana kuwathibiti viboko ndani ya bwawa la Mtera