Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Young Africans Yusufu Manji anatarajiwa kushiriki Mkutano Mkuu wa Wanachama wa klabu hiyo utakaofanyika Jumapili (Juni 27).

Manji amekamilisha mahitaji yote ili kuweza kushiriki Mkutano huo ikiwa ni pamoja na kulipia ada za uanachama wake.

Manji amelipia kadi yake ya Uanachama na kuthibitisha hatua hiyo kwa kusambaza picha ya risiti ya malipo, ambayo inaendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii.

Tangu aliporejea nchini mwezi uliopita, Manji amekua kimya kuhusu kurejea ndani ya klabu hiyo aliyoifadhili kwa kipindi cha miaka kadhaa, na hatua ya kulipia kadi yake ya Uanachama, imedhihirisha bado ana mapenzi ya dhati na Young Africans.

Uongozi wa Young Africans kupitia kwa Mwenyekiti wake Mshindo Mbette Msolla, umeitisha Mkutano Mkuu wa Wanachama, utakaofanyika mwishoni mwa juma hili jijini Dar es salaam, huku ajenda kuu ikiwa ni kupitishwa kwa rasimu ya Mabadiliko.

Mwigulu Nchemba: Makambo anarudi
UEFA EURO 2020: Ombi la Ujerumani lawekwa kapuni