Mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati Cesar Lobi Manzoki amewatoa wasiwasi Mashabiki na Wanachama wa Simba SC, kuhusu mpango wake wa kutua klabuni hapo.

Manzoki alitajwa sana mwanzoni mwa msimu huu na wakati wa Dirisha Dogo la usajili, kwa kuhusishwa na klabu ya Simba SC, lakini mpango huo ulishindikana.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Simba SC unaoendelea katika Ukumbi wa Mikitano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Mshambuliaji huyo amesema anaipenda klabu hiyo ya Msimbazi na ataitumikia siku moja.

Manzoki amesema anajua kuna baadhi ya watu waliwahi kumuhusisha na mpango wa kusajiliwa na timu inayovaa rangi ya Kinyoka Nyoka, lakini kwake hilo halipo, kwani kama kuna klabu ambayo anataka kuitumikia Barani Afrika kwa sasa, basi ni Simba SC.

“Naipenda Simba kuliko kila kitu. Najua kuna watu wengi walifikilia kuwa mimi nitavaa rangi ya kinyoka nyoka. Kama kuna klabu Afrika nataka kucheza basi ni Simba Sports Club.” amesema Cesar Manzoki.

Msimu uliopita Manzoki alikuwa akiitumikia Vipers SC ya Uganda na baadae aliuzwa kwenye Klabu ya Dallian International ya China.

Tuhuma mauaji ya raia: Polisi watano mbaroni, kitengo chafutwa
Simba SC kushiriki AFRICAN SUPER CUP