Miripuko ya risasi na mabomu, imeendelea kusikika katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum licha ya upande mmoja kudai kusitisha mapigano yaliodumu kwa siku ya nne ambayo yamesababisha vifo vya karibu watu 200.

Mapambano hayo ya kuwania madaraka, yalizusha mapigano kati ya vikosi vya majenerali wawili walionyakua mamlaka katika mapinduzi ya 2021, yaani mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan na naibu wake, Mohamed Hamdan Dagalo, ambaye anaongoza Kikosi cha Msaada wa Dharura, RSF.

Majenerali, Mkuu wa Jeshi, Abdel Fattah al-Burhan na Naibu wake, Mohamed Hamdan Dagalo.

Hatua hiyo, imepelekea wito wa kimataifa wa kukomesha uhasama uliosababisha kuongezeka kwa uasi, vifo na uharibifu huku Kamanda wa RSF, Dagalo, anayejulikana kama Hemeti, akitangaza kuunga mkono jitihada ya kimataifa ya kusitisha mapigano kwa masaa 24 huku upande wa jeshi la Sudani ukionekana kama kutotilia maanani jambo hilo.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema hadi sasa mapigano nchini Sudan, ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa Khartoum na maeneo mengine mbalimbali hayana dalili ya kusitishwa.

PICHA: Mashabiki Simba SC waanza safari ya Chalinze
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Aprili 19, 2023