Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema tayari rasimu za mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo na ile ya mitalaa zimekamilika na wakati wowote itatolewa kwa wadau, ili waone kilichopendekezwa na kutoa maoni yao.

Prof. Mkenda ameyasema hayo hivi karibuni Jijini Dodoma wakati akizungumza katika kikao cha kuwapitisha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo katika rasimu hizo.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda

Amesema, lengo la kufanya mapitio na mabadiliko hayo ni kutekeleza ahadi aliyotoa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kufanya mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 na mabadiliko ya mitaala ili kuwezesha kutoa elimu ujuzi na pia kuwezesha sera na mitaala kuakisi mahitaji ya sasa na baadaye.

“Kazi ya kwanza ya Kamati hizi ilikuwa kukusanya maoni ya wananchi na baadaye maoni hayo yalifanyiwa uchambuzi na kuwezesha kupatikana kwa rasimu ya mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo toleo la Mwaka 2023 na Rasimu ya Mitaala mipya,” amesema Prof. Mkenda.

Awali, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo Prof. Kitila Mkumbo aliishukuru Wizara kwa kuona umuhimu wa kuipitisha Kamati hiyo katika rasimu hizo ili nao waweze kutoa maoni yao.

Elimu maadili: Sheikh Kichwabuta awapa neno Wazazi, Walezi
Simba SC: Hatuchagui timu, aje yoyote