Ni takribani miezi sita sasa tangu kilipotokea kifo cha Muigizaji na mwanamuziki nguli wa muziki wa Hip hop Dunia, Earl Simmons, maarufu DMX, aliye fariki Dunia tarehe 9 Aprili, 2021.

Tangu afariki rapa DMX kumeibuka mijadala mbali mbali kuhusu mali za msanii huyo na namna zitakavyo gawanywa kwa mchumba pamoja na watoto wake .

Taarifa mpya zinasema kuwa pamoja na kuwa bado muafaka wa mgawanyo wa mali za rapa huyo haujapatika, inaelezwa kuwa kuna binti amejitokeza  na kudai kuwa yeye ni miongoni mwa watoto wa DMX, ambaye hakuwahi kutambulishwa kwenye familia.

Kwa mujibu wa Pagesix, binti huyo aitwaye Raven Barmer Simons mwenye makazi yake huko Georgia Marekani, aliwatafuta watoto wengine wa DMX na kuwaeleza ukweli wake kuwa na yeye ni mmoja wao.

Barmer-Simmons amejitokeza wakati ambao watoto wote wa DMX wako katika vita kali juu ya mali isiyohamishika ya rapa huyo yenye thamani ya Usd 1 milioni, ambayo hata baada ya ombi la mchumba wa marehemu DMX  Desiree Lindstrom kuwa msimamizi wa mali hiyo kukataliwa,

Pagesix  imeripoti Kuwa Jaji Helen Blackwood amewateua watoto watatu wa marehemu kuwa wasimamizi wa muda wa mali hiyo. Binti zake wawili wakubwa Sasha Simmons na Jada Oden pia walinyimwa nafasi ya kuwa wasimamizi.

“Jambo kubwa linalofuata ni kuamua ni nani warithi halali,” Herbert Nass, wakili wa amana na mashamba anayewasimamia watoto watatu wa wa marehemu DMX aliiambia Pagesix.

“Ugawanywaji wa mali hizo utaanza baada ya kukamilika kwa mchakato wa kuthibitisha uhalali wa watoto hawa kwa kupima DNA. Watoto wote halali wa DMX watastahili kupata sehemu sawa ya mali yake. Tunahitaji kukusanya mali na kulipa deni na gharama za utawala. Hatuna habari nyingi juu ya mapato yake, lakini sasa wasimamizi wa muda wameteuliwa, tunaweza kuuliza maswali na kutarajia majibu.” ameongeza wakili Herbert.

DMX alifariki tarehe 9 April, 2021 baada ya kupata mshtuko wa Moyo akiwa na umri wa miaka 50. Ambaye baada ya kifo chake, album yake ya nane kutoka ilifika kwenye nafasi ya 8 kwenye chati za muziki kubwa Duniani Billboard hot 200.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 25, 2021
Hakuna kuingia kwenye mahusiano bila mkataba