Kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Marc Wilmots amuunga mkono kocha wa Liverpool Jurgen Klopp kwa kudai kuwa mshambuliaji wa klabu hiyo Christian Benteke mwenye umri wa miaka 25 anahitaji kujifunza zaidi ili apate nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo.

Wilmots amesema haoni sababu ya kumlaumu kocha Jurgen Klopp na uongozi wa klabu hiyo kwa kushindwa kumuweka katika kikosi cha kwanza kwani mchezaji huyo ameshindwa kuonesha kiwango bora tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea Aston Villa mwaka 2015.

Kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji Marc Wilmots

“Najua anakosa raha ila ni wakati wa kujifunza na kufanya mazoezi kwa nguvu ili arejeshe kiwango chake na jukumu la mchezaji gani aanze lipo chini ya kocha” alisema kocha  Wilmots huku akisisitiza kuwa hata yeye ataumia kama mchezaji tegemeo atapungua kiwango ila cha muhimu ni kuangalia nani ataziba pengo lake ili maisha yaendelee.

Benteke ambae alinunuliwa kwa paun ml 32.5 na kocha alietimuliwa klabuni hapo Brendan Rodgers nakuwa mchezaji wapili kununuliwa kwa fedha nyingi katika historia ya klabu hiyo ameshindwa kuonesha thamani yake na hata katika timu ya taifa anaonekana hana nafAsi kubwa mbele ya mshambulaiji Romelu Lukaku ambae anafanya vizuri katika klabu ya Everton.

Arsene Wenger Aendelea Kukingiwa Kifua Ili Asiondoke
Roy Hodgson Ang'ang'ana Na Rooney