Mlinda mlango wa zamani wa klabu ya Arsenal, David Seaman amechoshwa na mtazamo hasi dhidi ya meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger  na ameonya kuwa mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi iwapo klabu hiyo  itamfuta kazi.

Wenger alitimiza miaka 20 akiwa na Arsenal mwezi Oktoba 2015 lakini alijikuta akiwa kwenye kiti cha moto wiki za hivi karibuni baada ya  The Gunners kuendelea kushindwa  kutamba  katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu na kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la FA.

“Nimechoshwa sana na habari za mtazamo hasi kuhusu Arsenal,” Seaman alinukuliwa akisema, “Mabadiliko ya kocha? kwangu hapana, mimi ni shabiki mkubwa wa Arsenal , Subiri tuone nini kitatokea mwisho wa msimu huu.,Tuone nini kimeenda tofauti tuweze kusahihisha ila kwangu mimi, mambo yapo sawa kabisa kwake.

Nimefanya naye kazi miaka saba mpaka minane na alikuwa mtu safi sana, nipo upande wa Arsene, daima nimekuwa nikisema hivyo na sina sababu ya kubadili akili yangu” Alisema David Seaman.

Seaman anaelewa ghadhabu za mashabiki wa Arsenal, lakini amewataka kubaki na mtazamo chanya na kuendelea kuwa na tumaini la mbio za ubingwa huku akisema kuwa hofu yake kama kocha huyo atatimuliwa huenda hali ikawa mbaya zaidi kama ilivyo kwa Manchester Utd baada ya kuondoka meneja wao mahiri Alex Ferguson.

 

“Inakera kuwa tumeanza  vizuri sana na tunapoteza katika ligi na katika Ligi ya Mabingwa Ilikuwa ni droo ngumu kupangwa na Barcelona, na bado kuna mwendo mgumu katika ligi, lakini, kama Leicester na Tottenham watapoteza pointi, nani ajuaye? Kujiamini ndio ushauri wangu amini katika kile unachokifanya,wameonesha kile wanachoweza kufanya watapiga hatua na huenda wakafikia malengo ya ushindi” Alimaliza David Seaman

 

Mwanakwetu Agoma Kurejea Nyumbani
Marc Wilmots Amkandamiza Benteke Kwa Kuungana Na Klopp