Marekani imezitaja nchi za China na Urusi kuwa ni tishio kubwa kwa usalama wa nchi hiyo huku ikiunda mkakati wa kujilinda dhidi ya nchi hizo.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Jim Mattis amezitaja China na Urusi kuwa ni nchi ambazo zinabadili itikadi za kisiasa na zinalengo la kuunda ulimwengu unaoendana na siasa zao zenye mlengo mmoja.
Aidha, mkakati huo wa usalama wa taifa, umeundwa kutokana na ishara ya Rais Donald Trump kujishughulisha na nchi za Urusi na China, huku akishinikiza kuboresha uhusiano na kuunganisha nguvu na Moscow na Beijing ili kuidhibiti Korea Kaskazini yenye silaha za nyuklia,
“Tutaendelea kutekeleza kampeni dhidi ya ugaidi ambayo tunashiriki wakati huu, lakini ushindani wa kuimarisha nguvu yetu, ndiyo kipaumbele cha usalama wa taifa letu,” amesema Mattis
-
Rais wa Palestina Abu Mazen azidi kumpinga vikali Trump
-
Daktari wa Ikulu Marekani atoa taarifa za uchunguzi akili ya Rais Trump
-
Umoja wa Afrika wamuita Trump kikaoni, kumuweka ‘kitimoto’
Hata hivyo, Urusi imesema kuwa sera hiyo ya Marekani ni ya Kibepari huku China ikisema kuwa hizo ni fikra za enzi ya vita baridi.