Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) imetangaza kusitisha msaada wa dola Milioni 472.8 ambazo ni sawa na takribani shilingi trillion moja, kutokana na uamuzi wa kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar pamoja na mwenendo wa zoezi la ukamataji unaotokana na sheria za makosa ya mtandao wakati wa uchaguzi.

Fedha hizo za zilikuwa zimelenga katika kusaidia sekta ya nishati na madini ikiwa ni pamoja na kuunganisha vijijini.

Balozi Mark B. Childress ametoa taarifa hii rasmi kwa serikali ya Tanzania:

Tarehe 16 Disemba, Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) haikuichagua Tanzania kwa mkataba wa pili. Bodi iliahirisha kupigia kura mkataba wa pili, ikisubiri kutatuliwa kwa masuala ya kiutawala.

Bodi inaweza kuangalia upya ustahilifu wa Tanzania mwaka 2016. Ninatumaini kwamba Serikali ya Tanzania itachukua hatua hivi karibuni zitakazotatua masuala hayo ya kiutawala. Halafu, Bodi itaweza kupiga kura kuichagua tena Tanzania na kuidhinisha maendeleo ya mkataba.

Masuala ya kiutawala ya Bodi yanaakisi maadili ya muda mrefu ya MCC. Kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa rais wa Zanzibar kulisitisha mchakato wa uchaguzi uliokuwa unaenda vizuri na kwa amani.

Matumizi ya Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 kuwakamata watu waliokuwa na kibali halali kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi yalikwaza uhuru wa msingi wa kujieleza na kukutana.

MCC imetiwa moyo na hatua zilizochukuliwa hivi karibuni na Rais Magufuli za kuimarisha vita dhidi ya ubadhilifu na rushwa. MCC inatumaini kuwa jitihada hizo zitaendelea na kuleta mabadiliko ya kimfumo.

Baada Ya Marekani Kupitia MCC Kusitisha Msaada Kwa Tanzania, Mbowe Amtaka Rais Magufuli Afanye Haya
Jose Mourinho Kuinoa Manchester United, Mpango waiva