Utawala wa Rais Joe Biden wa Ikulu ya White House umetangaza siku ya Jumatatu kuwa hakuna tena ulazima wa kuvalia barakoa muda wote raia anapokua eneo la Wazi na maeneo ya watu wengi ikiwemo maeneo ya viwanja vya ndege, ndani ya ndege, stesheni za Treni na ndani ya treni, vituo vya mabasi na sehemu nyinginezo bila kusahau katika magari ya abiria ya ‘Uber’.
Kulingana na mtandao wa NBC wa Marekani, Baada ya Jaji wa mahakama ya hakimu mkazi wa Florida Kathryn Kimball Mizelle, kutangaza kwa vituo vya kudhibiti magonjwa ya kuambukiza kuwa CDC Kuwa barakoa za kusafiria sio za lazima tena, ilipokelewa video moja mitandaoni ikionesha abria ambao wapo kwenye ndege wakifurahi pamoja waliposikia Rubani akitangaza hatua hiyo.
Hata hivyo sheria hiyo haijamlazimisha mtu kuacha kabisa kuvaa barakoa bali kila itu stava kwa utashi wake, na katika baadhi ya makampuni ya ndege wameendelea kuweka sheria kuwa wafanyakazi wa ndani ya ndege waendelee kuvaa Barakoa ikiwemo kampuni ya Delta.
Hata hivyo Upande wa Haki za Kijamii, umesema siku ya Humane kuwa utapeleka mashitaka Mahakamani ili kufungua kesi ya Kudhulumu haki ya afya kwa raia, wakiushitaki utawala wa Rais Biden na Ikulu ya White House na wakati huo bado wasafri hawatalazimishwa kuvaa Barakoa.
Secretary wa Ikulu ya White House, Jen Psaki alisema kuwa sheria hiyo ili ionekana imefanya kazi au haijafanya kazi inatakiwa kupewa walau siku 15 kuona kama maambukizi yataongezeka na kulazwa kwa wagonjwa wa Corona au Maisha yataendelea kama kawaida ingawa bado Utawala wa Ikulu unaamini sio lazima kuendelea na seria ya uvaaji wa ‘Mask’.
Alipoulizwa na Mwandishi wa NBC News kuhusu uvaaji wa Barakoa na ulazima wake kwa Raia, Rais Joe Biden wa Maremmani alisea ni ‘maamuzi ya kila mmoja’ na sio sheria ya taifa.
Kwa Muda wa Miaka miwili na zaidi, Marekani imekua na sheria ya uvaaja wa lazıma wa barakoa kila muda tangu kuibuka kwa maambukizi ya virusi vya Corona.