Meneja wa klabu ya Stoke City, Mark Hughes amesema anaamini kikosi cha Liverpool cha msimu huu, kinaweza kutwaa ubingwa wa PL, lakini akawatahadharisha kwa kutanabaisha kuwa inaweza kuwawia vigumu kama ukame wa taji hilo utawaandama kwa muda mrefu.

Kikosi cha Jurgen Klopp hadi juzi kilikuwa nyuma dhidi ya Chelsea lakini kilikuwa na mchezo mmoja mkononi kabla ya kuivaa Stoke siku mbili zilizopita.

Kikosi hicho pia hakijawahi kutwaa ubingwa tangu mwaka 1990 ambao ulikuwa ni wa 18 tangu kianze kushiriki michuano ya ligi kuu ya soka nchini England.

Kutokana na hali hiyo, Hughes ambaye aliwahi kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu akiwa mchezaji wa Manchester United amesema itakuwa ni kazi kubwa kumaliza ukame huo.

“Kila mwaka unakuwa mgumu zaidi, kila mwaka utazidi kuwa mgumu,” alisema kocha huyo.

Alisema kwamba wakati akichezea Man United alikuwa akizungumza hivyo mwanzoni, katikati na mwishoni mwa msimu.

Video: Majambazi wengi wanaotumia silaha wamekamatwa - Sirro
Young Africans Wasubiri Maamuzi Ya Kamati Ya Saa 72