Mmiliki wa mitandao ya kijamii Facebook, WhatsApp na Instagram Bwana Mark Zuckerberg amepoteza zaidi ya Tshs. Trilioni 13.8 na kupelekea kushuka mpaka nafasi ya 6 ya mtu tajiri duniani akitoka nafasi ya 5 kwenye orodha ya Watu matajiri zaidi duniani.

Hasara hiyo imekuja baada ya kukosekana kwa saa kadhaa kwa mitandao ya Facebook, WhatsApp, messanger na Instagram.

Mark Zuckerberg amewaomba radhi watumiaji wake kwa kusema anajua kiasi gani wanatumia huduma hiyo na walivyoteseka baada ya kutokuwa hewani kwa mitandao hiyo.

Facebook imeripoti kwa watumiaji wake kuwa ilikuwa inaweka vyema huduma zake na kwa sasa zipo vizuri na zimerudi hewani na Kampuni hiyo inasema sababu ilikuwa mabadiliko yaliyofeli ya mfumo.

Huduma zote tatu zinamilikiwa na Facebook na hazikuweza kupatikana kwenye wavuti au kwenye programu za simu za mkononi.

Downdetector, ambayo inafuatilia kukatika kwa huduma za mitandao ya kijamii ilisema ni hitilafu kubwa zaidi kuwahi kutokea, na ripoti milioni 10,6 za matatizo kutoka kwa wateja kote ulimwengun

Dar24 imezungumza na mtaalamu wa mitandao ya kijamii Maziku Kuwandu juu ya swala hili na amesema kuna wakati mifumo huweza kusimama na kila kitu kikashindikana kusuluhishwa kwa haraka.

Maziku amewasihi watumiaji wa mitandao hiyo jambo kama hilo linapotokea ni vizuri kuhakikisha wanapata ukweli na sababu za kukatika kwa mitandao kabla ya kujiingiza hasara ya kujiunga vifurushi au kuwaza kuwa simu zao zina matatizo.

Huduma zilikatika saa 16:00 GMT na watumiaji kuanza kupata huduma hizo karibu mwendo wa saa 02:00 GMT.

Agizo la Rais Samia tozo za mafuta
Kim Poulsen: Tutakusanya alama 9 nyumbani