Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, amezungumza na Wajumbe wa Tume ya Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Jeshi la Uhamiaji inayoshughulikia masuala ya Kiutumishi na Kiutendaji wa Askari katika Majeshi hayo, iliyofanyika Ukumbi wa Tanapa, jijini Dodoma.

Mazungumzo hayo yamefanyika hii leo Novemba 17, 2022 yakiwahusisha viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Hamad Masauni, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Maduhu Kazi pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Usalama vya Wizara hiyo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, akizungumza katika Semina ya Wajumbe wa Tume ya Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Jeshi la Uhamiaji.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Maduhu Kazi akizungumza katika Semina ya Wajumbe wa Tume ya Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Jeshi la Uhamiaji inayoshughulikia masuala ya Kiutumishi na Kiutendaji wa Askari katika Majeshi hayo, iliyofanyika Ukumbi wa Tanapa, jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati meza kuu) pamoja na Wajumbe wa Tume ya Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Jeshi la Uhamiaji wakisikiliza mada iliyowasilishwa na Afisa Sheria wa Wizara hiyo, Berious Nyasebwa kuhusu masuala ya Kiutumishi na Kiutendaji wa Askari katika Majeshi hayo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara hiyo, Flora Mrope alipokuwa akifafanua jambo kabla ya kuanza kwa Semina ya Wajumbe wa Tume ya Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Jeshi la Uhamiaji iliyofanyika Ukumbi wa Tanapa, jijini Dodoma, wa pili kushoto ni Naibu Waziri, Jumanne Sagini, wapili kulia ni Kaimu Katibu Mkuu, Dkt. Maduhu Kazi na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Miriam Mmbaga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Washindwa kuchagua Rais kwa mara ya sita
Ndege ATCL yashindwa kutua uwanja wa Bukoba