Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema kuwa kuna baadhi ya watu ambao wamepanga njama za kutaka kuichafua Serikali, hususani kuelekea kipindi hiki cha uchaguzi wa  Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa Urais 2019/2020.

Ameyasema hayo visiwani Zanzibar, wakati akizungumza na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani, juu ya hali ya usalama wa maeneo mbalimbali hususani kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Amesema kuwa kuna watu hawana nia njema na serikali hasa kuelekea kipindi hiki cha uchaguzi, na katika kufanya hivyo, wanatafuta mianya ya kupenyea, hivyo amewataka waliopewa dhamana mbalimbali kuacha mara moja kuweka mianya hiyo kwakuwa wanafanyakazi katika serikali ambayo haitakiwi kuchafuliwa.

“Tukitaka kuanzia sisi lazima tuondoe mianya yote ya watu wasiokuwa na nia njema na Serikali pamoja na wananchi wake ili wasiichafue.” amesema Masauni

Hivi karibuni akiwa visiwani humo Naibu Waziri Masauni aliitaka Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA, kuhakikisha inatoa huduma iliyobora kwa Watanzania.

 

Ashikiliwa na TAKUKURU kwa tuhuma za kuomba rushwa
Video: Daktari ataja sababu nane vifo vya ghafla, Siku 14 za kuvuna fursa