Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji, Japhet Hasunga ameutaka Uongozi wa Mkoa wa Simiyu kuanza mara moja utekelezaji wa mkakati kabambe uliozinduliwa Agosti 3, 2019 kuhusu Bima ya Mazao kwa wakulima.

Ametoa maagizo hayo wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Simiyu na kuhudhuriwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo kupokea maelekezo yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa kuhusu mustakabali wa zao la Pamba.

Hasunga amesema kuwa kuanza haraka kwa utekelezaji wa uandikishwaji wa wakulima kutaimarisha uwezekano wa kuboresha maisha ya wakulima ambao katika kipindi kirefu wameumia kupitia majanga mbalimbali wanayokumbana nayo ikiwemo mazao yao kuungua moto ama ukame.

Aidha, ameongeza kuwa uzinduzi wa Bima ya Mazao umefanyika katika mkoa wa Simiyu hivyo mkoa huo unapaswa kuanzisha haraka utekelezaji wake.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amempongeza Waziri wa Kilimo kwa kipindi cha muda mfupi ameweza kuonyesha dira na mwelekeo chanya katika ukombozi wa sekta ya kilimo nchini.

Mtaka ameongeza kuwa, maamuzi ya wizara ya kilimo inayosimamiwa na Waziri Hasunga ya kuanzisha Bima ya Afya, na Usajili wa wakulima ni miongoni mwa mambo muhimu yatakayoinua sekta ya kilimo nchini.

TPDC yatakiwa kusambaza Gesi mikoani
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Agosti 4, 2019