Mwanamziki wa marekani R kelly jana alitangaza kufanya onesho lake la kwanza tangu aachiwe kwa dhamana kufuatia kesi iliyokuwa ikimkabili.

Kwa mujibu wa ripoti ya TMZ hakufanikiwa kutumbuiza kutokana na idadi ndogo ya watu waliojitokeza kushuhudia tamasha lake.

Ukumbi aliokuwa anafanyia show yake ya kwanza unajulikana kama Dirty South uliamua kushusha bei ya tiketi, huku baadhi ya mashabiki wakipata nafasi ya kupiga nae picha (Selfie) na kufurahia kumuona japo imetafsiriwa kuwa kellz anaanza kupunguza mashabiki kutokana na maswahibu yanayoendelea.

Hata hivyo baadhi ya mashabki ambao walipata nafasi ya kuingia walitumia kiasi cha $50 hadi $100 kwaajili ya tiketi, walipata nafasi ya kushuhudia show ya sekunde 28 ya msanii huyo ambayo mashabiki waliomba kuimbiwa moja ya mstari uliopo kwenye nyimbo zake huku muda wote alitumia kuongea na mashabiki badala ya kufanya show.

Masaa machache kabla ya kuanza  show R kelly alionekana kwenye video  aliyoiposti kwenye instagram yake akiwaambia waandishi wa habari wakae mbali na yeye kwani ndivyo alivyoamaua kulipiza huku akisisitiza wakimuona wamuache, Alisema Kellz.

Kwa mujibu wa Tv na WRSP vimeripoti kuwa takribani watu 100 walijitiokeza kumpa kamapani kwenye klabu ya Springfield ambayo inauwezo wa kuingiza watu 450.

R kelly mwenye umri wa miaka 52 februari mwaka huu alishtakiwa kwa makosa 10 ya unyayasaji wa kingono kwa wasichana wanne waliokuwa chini ya umri wa miaka 18 kwa kipindi cha miaka 10 kuanzia mwishoni mwa mwaka 1990.

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Aprili 9, 2019
Mwili wa Nipsey kuagwa rasmi alhamisi

Comments

comments