Tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC imesema imemaliza kuhakiki matokeo ya uchaguzi wa marudio wa urais na inatarajia kutangaza hayo kutoka katika maeneo ambayo uchaguzi wa marudio ulifanyika.
Tume hiyo inatarajia pia kutoa mwelekeo kuhusu uchaguzi katika majimbo manne ya Magharibi mwa Kenya ambapo uchaguzi wa marudio uliahirishwa.
Naibu mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Kenya Consolata Nkatha amesema matokeo ya urais kutoka katika maeneo ambayo uchaguzi wa marudio ulifanyika yatatangwazwa saa tisa na nusu alasili.
-
Rais wa Iran ashikilia msimamo wake juu ya utengenezaji wa silaha
-
Al – Shabaab wasababisha ‘tumbua-tumbua’ Maafisa wa Somalia
-
Serikali yataifisha kundi la ng’ombe kutoka Rwanda
Consolata Nkatha amesema wagombea wote wa urais wamealikwa kuhudhulia katika shuguli hiyo japokuwa mgombea wa upinzani Raila Odinga alisusia uchaguzi huo.