Serikali ya Somalia imewafuta kazi maafisa wawili wa usalama wa ngazi za juu kufuatia shambulio la mabomu yaliyosababisha mauaji ya watu 27 Jumamosi iliyopita jijini Mogadishu, lililotekelezwa na kundi la kigaidi la Al -Shabaab.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini humo, Abdihakin Dahir Saiid na Mkurugenzi wa Intelijensia, Abdillahi Mohamed Sanbaloosh ndio waliokubwa na ‘tumbua-tumbua’ hiyo, saa chache baada ya tukio hilo la kigaidi.

Tukio hilo la Jumamosi limeripotiwa ikiwa ni wiki mbili tangu litokee shambulio lingine kubwa zaidi la kigaidi lililosababisha vifo vya watu 358.

Hata hivyo, kundi la Al – Shabaab ambalo linaushirika na kundi la Al Qaeda, limekanusha kuhusika na tukio la awali huku likikiri kuhusika na tukio la Jumamosi iliyopita.

Vyombo vya usalama vya Somalia vimeeleza lilifanikiwa kuwakamata magaidi watatu waliokuwa miongoni mwa waliotekeleza tukio la Jumamosi na kwamba magaidi wengine wawili walijilipua wenyewe baada ya kubaini kuwa wamezingirwa kila kona.

Video: JPM awapa ‘neno’ waliovunja nyumba ya CCM
Wageni wa La Liga waishangaza Real Madrid