Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amelitaka Jeshi la Kujenga Taifa kuwekeza katika kuwafundisha vijana matumizi ya teknolojia katika shughuli zake mbalimbali za uzalishaji mali na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Dkt. Mpango ameyasema hayo wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa na Maonesho ya JKT yanayofanyika katika Viwanja vya Suma JKT House eneo la Medeli Mashariki, Jijini Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango.

Amesema, ulimwengu wa sasa ni wakutumia teknolojia na akili zaidi kwa kuwa matumizi ya teknolojia yamedhihirisha uwezo mkubwa wa kuwezesha na kurahisisha utendaji kazi katika nyanja mbalimbalihuku akitoa Rai kwa JKT kuona umuhimu wa kuwatambua wataalam wake wabunifuni na kuwapa tuzo.

Aidha, amesema juhudi za kupanda miti na uhifadhi wa mazingira zifanywe na Kambi zote za JKT nchini, ili kuhakisha mazingira yanatunzwa kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho na kusisitiza juu ya matumizi ya nishati safi ili kupunguza ukataji miti ovyo.

Usajili wa Szoboszlaí waivuruga RB Leipzig
Robertinho atoa masharti ya usajili Simba SC