Kikosi cha Mbeya City FC  tayari kimetua mkoani Shinyanga tayari kwa mchezo wa duru ya lala salama ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya wenyeji Mwadui Fc, mchezo uliopangwa  kuchezwa  jumapili hii kwenye uwanja wa Mwadui  uliopo nje kidogo ya mji huu wa kanda ya ziwa.

Afisa habari na mawasiliano  wa   kikosi cha City, Dismas Ten amesema leo asubuhi kuwa nyota wote 18 waliosafiri kwa ajili ya mchezo huo wako kwenye hali nzuri kiafya na kinachosubiriwa ni dakika 90 za siku ya mchezo.

“Tumekuja hapa na wachezaji 18,wote wako kwenye hali nzuri kwa mujibu wa daktari wetu, asubuhi hii tumefanya mazoezi mepesi  na sasa tunasubiri siku ya mchezo,tunafahamu wapinzani wetu wana timu nzuri na pia wanacheza nyumbani, hilo halitupi shaka sana kwa sababu tuna kikosi ambacho kinaweza kushind popote, tumejiandaa vizuri na hilo ndiyo lengo letu”, alisema.

Kuhusu wachezaji waliosafiri kutoka jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo huo Ten  alisema kuwa City imelazimika kumuondoa kikosini mlinzi Hassan Mwasapili kutokana na kuwa na kadi tatu za njano  hivyo hawezi kuwa sehemu ya mchezo huo.

“Tumemuacha Mwasapili hii ni  kwa sababu ana kadi tatu za njano,kwa vyovyote tusingeweza kumtumia, badala yake  tumesafiri na Yusuph Abdalah mbaye amekuwa kwenye kiwango kizuri mazoezini  hasa baada ya kupona majeraha alisema Ten, huku akiwataja nyota wengine walio kwenye msafara huo kuwa ni  pamoja na – Juma Kaseja, Hanningtony Kalyesubula, John Kabanda,John Jerome,Yusuph Abdalah,Yohana Moriss,Tumba Sued,Haruna Shamte,Kenny Ally,Ramadhan Chombo,Raphael Daud, Geoffrey Mlawa,Salvatory Nkulula,Joseph Mahundi na wengine.

NORWAY KUENDELEZA ELIMU KWA WATOTO WA KIKE TANZANIA
Mesut Mustafa Ozil Kubembelezwa Kwa Mkataba Mpya