Msanii wa muziki wa kizazi kipya Maromboso amejitokeza hadharani na kuonesha machungu, baada ya Simba SC kupoteza alama tatu dhidi ya Young Africans jana Jumamosi (Julai 03), Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.

Maromboso ambaye ni shabiki wa Simba SC (Simba Lia Lia) ameonesha machungu yake kwa kuelekeza lawama kwa Mzee Haji Omar Shamte (Mzee Mpili).

Msanii huyo ameandika kwenye kurasa zake za kitandao ya kijamii: “Daah..!! Mzee Mpili Kwani Tulikukosea nini Sisi WanaMsimbazi ….?”

Huenda Mbosso ameelekeza lawama hizo kwa Mzee Mpili kufuatia harakati za kizalendo kwa klabu yake ya Young Africans alizozionesha kabla ya mchezo dhidi ya Simba SC alipohojiwa na Dar24 Media #taarifabilamipaka tangu mwanzoni mwa juma hili.

Katika mahojiano na Dar24 Media #taarifabilamipaka Mzee Mpili alisema: “Simba hawatufungi, hawana mpira wa kuifunga Yanga, ninakuhakikishia hawatufungi.”

“Nimejiandaa kisawa sawa, nina watu wa kufanya kazi ya kuizuia Simba isitufunge Jimamosi (Julai 03).”

Ushindi wa jana Jumamosi (Julai 03) umeiwezesha Young Africans kufikisha alama 70, huku ikisaliwa na michezo miwili mkononi kabla ya kumaliza msimu huu 2020/21 baadae mwezi huu.

Simba SC yenye alama 73 inaendelea kubaki kileleni mwa msimamo, huku ikibakiza michezo minne mkononi kabla ya kumaliza msimu huu 2020/21 baadae mwezi huu.

Fedha zitakozopelekwa si chini ya asilimia 50 - Dkt Nchemba
Mwakalebela auota ubingwa Young Africans