Makamu Mwenyekiti wa Young Africans Fredrick Mwakalebela amesema ushindi wa jana Jumamosi (Julai 03) umefufua matumaini ya kutwaa ubingwa licha ya timu yao kuendelea kuwa nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Young Africans imefikisha alama 70 kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya watani zao jadi Simba SC wanaoendelea kuongoza kwa alama 73.

Mwakalebela ambaye aliondolewa kifungo cha miaka mitano kujihusisha na soka mwishoni mwa mwezi Juni amesema: “Mbio za Ubingwa bado zinaendelea, sisi hatuhesabu point ambazo ziko hewani, tunahesabu point zilizoko mkononi.

“Tulisema tunahitaji makombe matatu, moja tulishaliweka mkononi, lingine ndo hili tunakimbizana nalo, na lingine lipo Kigoma,”

Young Africans imebakiza michezo miwili kuelekea mwishoni mwa msimu huu na kama watashinda yote watafikisha alama 76.

Simba SC imebakiza michezo minne mkononi na kama itashinda yote itafikisha alama 85.

Kama Young Africans itahitaji kuwa bingwa, italazimika kuiombea mabaya Simba SC kupoteza michezo yao yote, na wao washinde iliosalia.

Mbosso amlilia Mzee Mpili
TMA: Upepo mkali kuathiri maeneo yafuatayo