Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania  (TMA) imetoa tahadhari ya upepo mkali kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani wa Bahari ya Hindi kwa siku tano zijazo.

Hayo yamesemwa na Meneja Samweli Mbuya ambapo amesema kuwa upepo huo unaotarajiwa kuwa wa kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2.

Amebainisha maeneo yanayotarajiwa  kuathirika  na wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhali ni mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani pamoja na  visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba.

 “Sisi tunafuatilia mifumo ya hali ya hewa na jinsi ambavyo tumeona kuna uwezekano  kuanzia Julai 7, 2021 kasi ya upepo itaongezeka na kusababisha mawimbi makubwa kwa eneo lote la ukanda wa Bahari ya Hindi,” amesema Mbuya

Amesema athari zinazoweza kujitokeza kutokana na hali hiyo  ni  kuathirika kwa baadhi ya shughuli za usafirishaji na uvuvi na kuwaomba wananchi kuendelea kufuatilia mwenendo wa taarifa za hali ya hewa kwa sababu hiki ni kipindi cha kipupwe .

Mwakalebela auota ubingwa Young Africans
Waziri Mulamula atoa siri chanjo ya corona, uongozi wa Rais Samia (Video)