Watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango wametakiwa kuhakikisha kuwa hakuna Wizara ama Taasisi itakayo pelekewa bajeti yake ya maendelelo chini ya asilimia 50 katika bajeti ya Serikali iliyoanzwa kutekelezwa kuanzia Julai 1, mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, wakati akizungumza na watumishi wa Wizara hiyo ambapo pamoja na mambo mengine ametoa mwelekeo wa utekelezaji wa Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2021/2022.

“Nataka mkasimaie ugawaji wa rasilimaji fedha kwa kila Wizara ili tukirudi tena bungeni kuelezea utekelezaji wa bajeti kusiwe na mahali ambapo fedha za maendeleo zitakuwa zimepelekwa chini ya asilimia 50” amesema Dkt. Nchemba.

Dkt nchemba amewaagiza watumishi hao kujiwekea utaratibu wa kufuatilia kwa umakini utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo inayotokana na fedha zinakazotolewa na Serikali ili kuona utekelezaji wake na kama zimetumika kama ilivyokusudiwa kwa kuwa itasaidia miradi kukamilika kwa wakati.

Aidha, aliwataka watumishi hao kuendelea kufanya kazi kwa weledi mkubwa kwa kuzingatia maadili, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma.

Mashabiki Simba SC wamchefua Manara
Mbosso amlilia Mzee Mpili