Mwenyekiti wa Chama Demokrasia na Maendeleo (Chedema), Freeman Mbowe amepinga suala la lililotolewa na Dkt. John Magufuli la kuwapeleka madaktari 500 nchini Kenya.
Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam wakati wa kikao cha uchaguzi wa Viongozi wa Kanda ya Pwani wa chama hicho, Mbowe amesema kuwa Rais Magufuli hapaswi kupeleka madaktari nchini humo badala yake ahakikishe anatoa ajira kwa madaktari hao.
“Sisi kama Chadema tunapinga vikali agizo la Rais kupeleka madaktari nchini Kenya hili hali anajua kuwa kule hali si shwari, tunamtaka awapatie ajira madaktari hao,”amesema Mbowe.
Aidha, Mbowe amesema kuwa wao hawazuii mtu kwenda Kenya kufanya kazi kama hali ya nchi ni shwari, lakini kwa sasa hakuna sababu ya Serikali kuruhusu kwenda kufanya kazi Kenya.
Hata hivyo, amesema kuwa ni vyema Serikali ikaweka wazi kuwa wameshindwa kuajiri madaktari wataeleweka lakini si kufanya mchezo huo.
Juzi Rais John Magufuli alimtaka Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kuharakisha mchakato wa kupatikana kwa madaktari hao.