Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa leo Februari 13, 2022 anatarajia kushiriki kwenye kilele cha Tamasha la kimataifa la Sauti za Busara la mwaka huu mjini Zanzibar.

Tamasha la Sauti za Busara ni miongoni mwa matamasha makubwa nchini ambayo yamefanikiwa kuonesha utamaduni wa nchi duniani kupitia sanaa za muziki.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi ambaye anashiriki amesema tamasha la mwaka huu limeboreshwa zaidi ukilinganisha na miaka ya nyuma.

Aidha, amesema kutokana na tamasha hili amejifunza mengi ambayo yanaweza kusaidia kuboresha matamasha yanayokwenda kuandaliwa hivi karibuni.

“Tumejifunza mengi katika tamasha hili, kazi iliyo mbele yetu ni kubeba mambo mazuri ya tamasha hili kuboresha matamasha yanayokuja mbele yetu yawe kwenye hadhi ya kimataifa ili kuitangaza Tanzania na kuuza utamaduni wetu duniani kama tulivyo elekezwa na Rais wetu, Samia Suluhu Hassan”. Ameongeza Dk. Abbasi

Pia katika tamasha hili Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa Dkt. Emmanuel Ishengoma ameshiriki.

Awali Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika Tamasha la Utamaduni la mkoa wa Kilimanjaro alielekeza Wizara ya utamaduni, Sanaa na Michezo kushirikiana na wadau kuandaa matamasha makubwa ambayo yatasaidia kutangaza utalii na utamaduni wa Taifa la Tanzania kimataifa.

Hivi karibuni Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Alli Mwinyi ameliezea Tamasha la Sauti za Busara kuwa lina mchango muhimu wa kuhamasisha umoja na mshikamano nchini.

Mikel Arteta amjibu Aubameyang
Peter Msechu ndani ya Zima moto